MSAADA

Ramani ya huduma zinazosaidia na kutetea walemavu.

Kutembea Pamoja, Kutembea Mbali

Katika safari yetu maishani, sote twaihitaji msaada kutoka kwa wenzetu. MSAADA uliundwa kupeana habari inayoaminika na kupatikana kwa urahisi kuhusu rasilimali za ulemavu kote Kenya. Kwa kuwaunganisha walemavu kwa rasilimali zinazofaa na msaada, tunatarajia kutembea pamoja nao katika safari yao ya afya na ustawi.

Tafadhali kumbuka: Hizi rasilimali zimepatikana kwenye vitabu vya habari (saraka), wavuti ya serikali na kwa mawasiliano ya moja kwa moja. AMPATH haiidhinishi shirika lolote iliyoorodheshwa na kujumuishwa kwenye ramani hii ya rasilimali.

Supporters_Gray_Sm.png

Rasilimali Zaidi Zinazotakikana

Je, shirika lako linapeana huduma kwa walemavu?

 

TIMU YETU

Dr. Eren Oyungu

Profesa msaidizi wa afya ya watoto

Chuo kikuu cha Moi, Shule ya kidaktari

Na mafunzo ya ziada kwa neurolojia, Mazoezi ya kliniki ya Dr. Oyungu inazingatia kwa ujumla, afya ya watoto na pia ugonjwa wa kifafa kwa watoto na ulemavu utotoni. Dr. Oyungu anawafunza wanafunzi masomo ya kidaktari na wasajili wa watoto katika Chuo kikuu cha Moi na pia kufanya utafiti kwa kushirikiana na mtandao wa utafiti, AMPATH (AMPATH Research Network) iliyoko Kenya.

Dr. Megan McHenry

Profesa msaidizi wa sekta ya watoto

Chuo kikuu cha Indiana, Shule ya kidaktari

Utafiti wa Dr. McHenry unazingatia afya ya watoto kimataifa, mvuto wake sana sana ikiwa ni kwa maendeleo ya kineurolojia kwa watoto waliozaliwa na wazazi waliyoathiriwa na virusi vya ukimwi na pia utekelezaji wa sayansi. Anafanya utafiti kwa kushirikiana na Dr. Oyungu kwa mtandao wa utafiti wa AMPATH (AMPATH Research Network) iliyoko Kenya.

Michael Musili

Muundaji mwenza wa MSAADA

Miaka ya Sita, Chuo kikuu cha Moi, Shule ya kidaktari

Mwaka wa 2018 alikuwa kati ya wanafunzi wanne wa kwanza katika shule ya kidaktari kuchaguliwa kuenda Indiana kwa mpango wa kubadilishana. Ana ujuzi wa utafiti baada ya kufanya masomo kadhaa na pia kufanya na AMPATH kama msaidizi wa utafiti mwaka wa 2019. Ana hamu ya upasuaji na ndoto za kuwa mpasuaji wa moyo na kifua.

Mary Ann2.png

Mary Ann Etling

Muundaji mwenza wa MSAADA

Miaka ya Pili, Chuo kikuu cha Indiana, shule ya kidaktari.

Mwaka wa 2018 alipokea tuzo ya Fulbright Research kujifunza kuhusu vizuizi zinazoathiri watunzaji wa watoto walemavu, kaskazini mwa Uganda. Anafanya na AMPATH kama msomi wa Slemanda. Anatumai kufanya masomo kuhusu watoto na afya ya kimataifa.

BlueSquare.png